Baada ya kumaliza msiba wa mkewe hayati Mercy Chama, kiungo mahiri wa Simba na timu ya Taifa ya Zambia, Clatous Chama amewashukuru wadau wote waliokuwa nae bega kwa bega katika kipindi chote cha majonzi
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Chama ameweka ujumbe maalum wa shukrani kwa familia yake ya klabu ya Simba pamoja na wadau wote waliomfariji
Wiki chache zilizopita zimekua ngumu sana kwangu na familia yangu baada ya kuondokewa na Mpendwa wetu Mercy lakini yote kwa yote tunamshukuru Mungu mwenye sababu ya kila kitu kinachotokea maishani mwetu
Siku hizi za majonzi zingekua ngumu zaidi kama isingekuwa msaada wenu wa dhati ambao mmekua mkinipatia
Mmelia na mimi na zaidi ya yote mmeniombea na nathubutu kusema kuwa maombi yenu yametufariji mimi na familia yangu kwa kiasi kikubwa
Nipende kuushukuru uongozi wa Simba Sc chini ya Mo Dewji na Barbara Gonzalez kwa kunishika mkono katika kipindi ambacho nilikuwa nikiwahitaji zaidi
Shukrani za dhati ziwaendee Wachezaji wenzangu na Mashabiki wa mpira ulimwenguni kote kwa kuwa na mimi bega kwa bega
Amani ya milele imuangazie Mke wangu mpendwa, hayupo kimwili lakini tupo nae kiroho na anaishi miongoni mwetu kila siku