Hakufanya vizuri sana kwenye mchezo wa robo fainali ligi ya mabingwa dhidi ya Kaizer Chiefs na kupelekea mashabiki wamtishwe zigo la lawama
Lakini kwa hakika Chris Mugalu ni miongoni mwa washambuliaji bora sana wanaoweza kutumika katika majukumu tofauti uwanjani
Leo katika mchezo dhidi ya Namungo Fc, Mugalu alihusika kattika mabao mawili akifunga moja na kusaidia bao la pili lililofungwa na nahodha John Bocco
Mugalu ni mshambuliaji msumbufu ambaye wakati wote anazunguka katika eneo la upinzani, utamuona upande wa kulia, kushoto, katikati, yuko kila mahali!
Leo amefunga bao lake la tisa msimu huu
Kocha Didier Gomes anapendelea kumtumia Mugalu kwa sababu anaweza kumtumia katika majukumu tofauti uwanjani
ADVERTISE HERE