Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amesema hana tatizo lolote na mshambuliaji Meddie Kagere
Aidha Gomes amesema hafahamu chochote kuhusu tuhuma zilizotolewa na wakala wa mchezaji huyo Patrick Gakumba
Gomes amesema Kagere ni mshambuliaji anayefanya vizuri kama ilivyo kwa wenzake John Bocco na Chris Mugalu
Lakini ni yeye mwenye jukumu la kuamua ni yupi atacheza wakati gani
"Sitaki kuongelea kuhusu matatizo ya Patrick Gakumba, sijui chochote kuhusu malalamiko yake na siwezi kuzungumzia"
"Binafsi Sina tatizo na mshambuliaji wangu (Kagere), wiki tatu zilizopita nilizungumza na washambuliaji wote watatu (Kagere, Bocco na Mugalu) kwamba wanatakiwa kukubali na kuheshimu maamuzi yangu"
"Kuna wakati Bocco atacheza, kuna wakati Kagere atacheza na kuna muda watacheza washambuliaji wawili"
"Mechi dhidi ya Mwadui Kagere alianza baadaye akingia Bocco. Sijasikia malalamiko yoyote kutoka kwa wachezaji wangu na wanafahamu kama wanataka kulalamika wanajua mlango wangu upo wazi wanaweza kuzungumza na mimi sio meneja"
"Kila mtu anafahamu Kagere anafanya kazi nzuri, mimi sina tatizo na mtu yeyote," alisema Gomes
Hii sio mara ya kwanza kwa Gakumba kuwashushia lawama makocha pale anapoona Kagere hapati nafasi ya kucheza mara kwa mara
Aliwahi kufanya hivyo wakati wa Sven Vandenbroeck. Uongozi wa Simba umemtaka Gakumba aheshimu maamuzi ya kocha kwani hana mamlaka ya kuingilia masuala ya benchi la ufundi