Klabu ya Kaizer Chiefs kutoka Afrika Kusini inatarajiwa kuwasili nchini leo tayari kwa mchezo wa mkondo wa pili robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa dhidi ya mabingwa wa Tanzania, Simba
Pamoja na kutotoa taarifa juu ya ujio wao, timu hiyo inatarajiwa kuwasili jioni na siku ya kesho watafanya mazoezi kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa
Chiefs wamekuwa na hofu pengine ni kutokana na mwenendo wa matokeo ya Simba inapokuwa nyumbani wakidhani wakija mapema watafanyiwa hujuma
Jana Afisa Habari wa Simba Haji Manara alisema pamoja na kuwa wao hawakuwatendea haki mashabiki wao waliokuwa kwenye msafara wa Simba kule Afrika Kusini, wao hawatawawekea kipingamizi
Mchezo dhidi ya Chiefs utapigwa kuanzia saa kumi kamili alasiri
ADVERTISE HERE