Winga wa Simba Bernard Morrison ameondoka jijini Dar es salaam mapema kuelekea Afrika Kusini kuungana na wenzake wanaoendelea na maandalizi ya mchezo wa robo fainali ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs
Mchezo huo utapigwa Jumamosi, May 15, uwanja wa FNB huko kwa Mzee Madiba
Morrison anakwenda kukiongezea nguvu kikosi cha kocha Didier Gomes ambaye amepania kupata ushindi ugenini ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga nusu fainali
Morrison atakuwa silaha muhimu kwa Simba katika mchezo huo kwani amewahi kucheza soka hapo Afrika Kusini kwa mafanikio makubwa
Aliitumikia klabu ya Orlando Pirates kwa misimu mitatu kabla ya kuelekea DR Congo kujiunga na DC Motema Pembe
ADVERTISE HERE