Morrison anasubiri adhabu Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Jul 2020
Morrison anasubiri adhabu Yanga

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema uongozi wa timu hiyo utamchukulia hatua winga Bernard Morrison kufuatia kitendo chake cha kukacha kukaa kwenye benchi baada ya kufanyiwa mabadiliko katika mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho dhidi ya Simba

Katika mchezo huo ambao Yanga ilikubali kipigo cha mabao 4-1, baada ya kufanyiwa 'sub', Morrison 'alimvimbia' mwamuzi pale alipojaribu kumzuia asiondoke eneo la uwanja na hata kumsukuma na kuelekea katika vyumba vya kubadilishia nguo na kisha kuondoka moja kwa moja kwa usafiri wa Bodaboda

Mwakalebela amesema Morrison ataitwa mbele ya Kamati inayohusika na masuala ya Nidhamu ndani ya klabu ya Yanga na atachukuliwa hatua kulingana na makosa yake

"Hakuna aliyefurahishwa na tukio lililofanywa na mchezaji wetu Bernard Morrison kwenye mchezo dhidi ya watani zetu Simba. Akiwa mchezaji wa Yanga mwenye mkataba halali, tutakaa nae na kumsikiliza kisha ataadhibiwa kulingana na makosa aliyofanya," alisema Mwakalebela

Kumekuwa na presha kubwa kutoka kwa mashabiki wa Yanga ambao wengi wameonyesha kutomuhitaji tena mchezaji huyo katika timu yao

Mwanachama na Mhamasishaji maarufu Jimmy Msindo 'Kindoki', amesema yeye kama shabiki kindakindaki wa Yanga hatakuwa tayari kuingia uwanjani kuishabikia timu yake kila itakapotokea jina la Morrison litakuwa miongoni mwa wachezaji wanaoshuka uwanjani

Kindoki amemtaka Mghana huyo kujitokeza hadharani kuwaomba radhi mashabiki wa Yanga kwa matukio yake ya utovu wa Nidhamu na aahidi hatayarudia tena, wanaweza kumsamehe

Wiki iliyopita, Morrison aliingia katika mvutano na uongozi wa Yanga akikana kuongeza mkataba wa miaka miwili. Hata hivyo madai yake yaligonga mwamba TFF

Alijiunga na Yanga usajili wa dirisha dogo mwezi Januari akisaini mkataba wa miezi sita ambao unamalizika leo Julai 14

Baada ya kuridhishwa na uwezo wake, uongozi wa Yanga kupitia wadhamini wao GSM, walimuongeza mkataba wa miaka miwili akilipwa zaidi ya Tsh Milioni 70

Nyota huyo 'alivurugwa' baada ya kupata ofa kutoka klabu moja huko Arabuni iliyokuwa imemuahidi kumlipa mshahara wa zaidi ya Dola 15,000 kwa mwezi

Lakini pia Yanga ilipeleka malalamiko TFF ikidai kuwa na ushahidi klabu ya Simba 'kumrubuni' mchezaji huyo ili ajiunge nao

Morrison mwenyewe alithibitisha kupewa dola 5,000 na aliyemtaja kuwa Wakala wa klabu ya Simba, fedha hiyo akipewa kama sehemu ya ushawishi ili asaini mkataba wa Simba

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’