Kikao cha pamoja kati ya Wizara, TFF, Bodi ya Ligi na viongozi wa klabu za Yanga na Simba kimefikia makubaliano ya kurudiwa kwa mchezo kati ya Simba dhidi ya Yanga uliokuwa upigwe Jumamosi iliyopita kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo baada ya maagizo ya Serikali hapo jana, imeweka bayana maamuzi yaliyofikiwa pamoja
Ni kuwa mchezo huo utarudiwa ili kuwapa mashabiki kile walichokihitaji. Tarehe mpya ya mchezo huo itapangwa na Bodi ya Ligi
Mashabiki wote 43,947 waliongia uwanjani watarejeshewa tiketi zao ili waingie kwenye mechi ijayo itakayopangiwa tarehe.
Pia mashabiki wapya watauziwa tiketi kwa idadi inayoruhusiwa
Aidha maazimio mengine ni kuitishwa kikao cha kuondoa changamoto zilizopo baina ya klabu ya Yanga na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
