Gomes kuwatumia Yanga kuwapa salamu Chiefs

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
7 May 2021
Gomes kuwatumia Yanga kuwapa salamu Chiefs

Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amesema atatumia mchezo dhidi ya Yanga kama sehemu ya maandalizi ya kikosi chake kuelekea mchezo wa robo fainali ya ligi ya mabingwa dhidi ya Kaizer Chiefs ambao utapigwa wiki ijayo Afrika Kusini

Kesho 'Mnyama' Simba atashuka kunako dimba la Benjamin Mkapa kuwakabili watani zake Yanga katika mchezo ambao Wanamsimbazi wanajua alama zote tatu ni zao wasichofahamu ni idadi ya mabao tu!

Gomes amesema chake ni lazima kiibuke na ushindi kutokana na maandalizi mazuri waliyofanya, lakini pia ubora wa wachezaji wake.

Hata hivyo, alisema pambano hilo litakuwa mgumu, lakini kutokana na mbinu alizowapa wachezaji wake mazoezini, ana amini watapata matokeo ambayo yatazidi kuwaweka kwenye mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wao.

"Ni mchezo mgumu kucheza na mpinzani wako kwenye ligi siyo jambo dogo lolote linaweza kutokea sababu tunakutana na timu yenye malengo kama yetu ya kutwaa ubingwa, lakini najivunia ubora wa wachezaji wangu na maandalizi tuliyofanya na kiwango tulichonacho hivi sasa hasa ikizingatiwa tumepata uzoefu mkubwa kupitia mechi za kimataifa," alisema Gomes

"Mchezo dhidi ya Yanga pia utatusaidia kama sehemu ya mazoezi kuelekea mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika  dhidi ya  Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini"

Gomes alisema amewafuatilia Yanga kwenye mechi mbili walizocheza hivi karibuni ikiwamo dhidi ya Tanzania Prisons na amepata mbinu za kuwadhibiti ingawa anatarajia watabadilika zaidi kutokana na kuwa chini ya kocha mpya Nabi ambaye ameiongoza timu hiyo kwenye mechi mbili tu mpaka sasa.

Alisema mpaka sasa jeshi lake lote lipo sawa kuelekea mchezo huo na wachezaji wamemwonesha matumaini makubwa ya kupata pointi zote tatu mbele ya Yanga ambayo imepoteza michezo miwili kama walivyo wao.

Gomes alisema ingawa yeye ni mara yake ya kwanza kukutana na Yanga akiwa kocha wa Simba, tayari ameona presha ilivyokuwa juu kwa mashabiki, wachezaji na hata baadhi ya viongozi  hivyo amepanga kuhakikisha anawapa furaha na yeye kuingia kwenye rekodi ya kuifunga Yanga.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Goli la ushindi dhidi ya Fountain Gate; FT : Fountain Gate 0-1 Simba
Goli la ushindi dhidi ya Fountain Gate; FT : Fountain Gate 0-1 Simba
17m ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Fountain Gate 1-0 Tanzanite Kwaraa
Simba mwendo mdundo, yaichapa Fountain Gate 1-0 Tanzanite Kwaraa
36m ago
READ MORE β†’
Kikosi : Fountain Gate vs Simba, NBC PL, Oct 29
Kikosi : Fountain Gate vs Simba, NBC PL, Oct 29
3h ago
READ MORE β†’
Kamati ya uchaguzi Simba imesisitiza, mchakato unaendelea
Kamati ya uchaguzi Simba imesisitiza, mchakato unaendelea
4h ago
READ MORE β†’
Mangungu aibuka, apinga mchakato wa uchaguzi Simba
Mangungu aibuka, apinga mchakato wa uchaguzi Simba
6h ago
READ MORE β†’
Tutapambana tuvuke mtoano - Barker
Tutapambana tuvuke mtoano - Barker
7h ago
READ MORE β†’
Matchday; Fountain Gate vs Simba, NBC PL
Matchday; Fountain Gate vs Simba, NBC PL
9h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
12h ago
READ MORE β†’
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’