FT : Kagera Sugar 0-1 Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Jul 2020
FT : Kagera Sugar 0-1 Yanga

Licha ya kucheza mbele ya mashabiki wake, Kagera Sugar leo imeshindwa kufurukuta mbele ya Yanga baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Kaitaba

Baada ya kutoa upinzani mkali kwenye mchezo wa robo fainali kombe la FA, wengi waliamini mechi ya leo isingekuwa rahisi kwa Yanga lakini mabingwa hao wa kihistoria wamedhihirisha mkubwa ni mkubwa tu

Bao la Bernard Morrison aliloweka kambani kwenye dakika ya 77 baada ya pasi ya Yikpe, lilitosha kuihakikishia Yanga ushindi muhimu ambao unawaweka katika nafasi nzuri kabla ya mchezo dhidi ya Simba Julai 12

Yanga leo ilikuwa bora kuanzia eneo la mlinda lango Farouk Shikhalo aliyeokoa nafasi kadhaa za wazi

Vijana wa Luc Eymael walishambulia kwa kasi na kuzuia pamoja pale walipopoteza mpira na hivyo kuwapa wakati mgumu Kagera Sugar kuweza kumfikia Shikhalo kwa urahisi

Ushindi huo umeirudisha Yanga katika nafasi ya pili, wanaweza kubaki katika nafasi hiyo kutegemeana na mtokeo ya mchezo kati ya Azam dhidi ya Mwadui Fc

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’