Simba kamili kuivaa Stand United leo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
2 Mar 2018
Simba kamili kuivaa Stand United leo
Vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba wanashuka dimbani kuwakaribisha Stand United katika mechi ya ligi hiyo itakayofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kocha msaidizi wa Simba Masoud Djuma, amesema kuwa kikosi chake kiko tayari kwa mchezo huo na kuongeza kuwa wataikaribisha Stand United kwa tahadhari.

Djuma amesema kuwa kila mechi ina mbinu zake na hawataki kuikabili timu kwa kuangalia historia ya mechi iliyopita kwa sababu timu zinabadilika na wachezaji wanakuwa tofauti kulingana na mazingira ya sasa.

Kocha huyo amesema, mbali na kuwajenga stamina, wanawaambia wachezaji wapambane kupata ushindi katika dakika 90 zilizopo na wasifikirie mechi zao zinazofuata au za wapinzani wao.

"Kila mara tunawaambia tuangalie mechi yetu, tupige hesabu za pointi zetu na si za wengine, hapa tulipo kama tunashinda mechi zote hakuna atakayetukamata na hivyo tutakuwa mabingwa, tuko mbele hata tukicheza mechi nyingi na kushinda ni faida kwetu," alisema Djuma.

Aliongeza kuwa suala la mabadiliko ya ratiba kwa nchi za Afrika ni la kawaida na kuwataka wachezaji wake wawe tayari kwa mapambano wakati wowote mpaka mechi yao ya mwisho ya kumalizia msimu.

"Hakuna mechi rahisi na ligi ndio inazidi kuwa na ushindani, kuna wanaowania ubingwa na vita kubwa ni ile ya wanaotaka kushuka daraja, timu zote hizi tunakutana nazo, kikubwa ni kupambana na si kukata tamaa, Mungu akipenda tutatimiza kile tunachokitafuta," Djuma aliongeza.

Naye Kocha wa Stand United, Athumani Bilo, amesema kuwa Simba ni timu kubwa lakini wanapokuwa uwanjani wote wanafanana na kikubwa ni wachezaji wake kuhakikisha wanatumia vyema nafasi watakazopata katika mchezo huo.

"Tumekuja kusaka pointi, lengo letu ni kushinda na hii inawezekana, hakuna kigezo cha kila mmoja anashinda nyumbani kwake, hata ugenini inawezekana," alisema kocha huyo.

Baada ya mechi ya leo, Simba itaanza maandalizi ya kuwakaribisha wapinzani wao katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Al Masry kutoka Misri, watakutana Machi 7 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’