Simba yapuuza 'propaganda' za Kwasi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
4 May 2021
Simba yapuuza 'propaganda' za Kwasi

Uongozi wa Simba umefunguka kuhusu zile tetesi za kufungiwa kufanya usajili kwa kipindi cha msimu mmoja na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa)

Taarifa hizo za kufungiwa Simba zilienea hivi karibuni kwa kile kilichotajwa kushindwa fidia za kuvunja mkataba wa aliyekuwa beki wao wa pembeni, Mghana Asante Kwasi

Katika taarifa hiyo ilielezwa Simba imefungiwa baada ya kushindwa kumlipa fidia ya Sh 9Mil baada ya kuvunja mkataba wa kuendelea kuichezea timu hiyo

Mkuu wa Kitengo cha Maudhui cha Simba, Ally Shatry alisema kuwa hizo taarifa hazina ukweli wowote za wao kufungiwa huku akiwataka mashabiki wa timu hiyo kuachana nazo

Shatry alisema kuwa, hizo ni proganda zilianzishwa kwenye mitandao ya kijamii zenye lengo la kuwaondoa kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara

Aliongeza kuwa hakuna barua yoyote ya kiofisi waliyopokea kutoka Fifa kuhusiana na taarifa hizo, kama zingekuwa za kweli basi wangeandikiwa barua na shirikisho hilo

"Kinachoendelea sisi tunakijua kila kitu, hizo ni propaganda zenye lengo baya za kutuchafua na kututoa kwenye mbio zetu za ubingwa wa ligi"

"Katika kuthibitisha hilo hakuna barua yoyote tuliyopokea kutokea Fifa hata hilo shirikisho hilo halifanyi kazi na mitandao ya kijamii iliyovumisha taarifa hizo. Kama uongozi tumezipuuza taarifa hizo na badala yake nguvu na akili zetu tunazielekeza katika mchezo ujao wa ligi ," alisema Shatry

Alipotafutwa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania 'TFF', Cliford Ndimbo kuhusiana na ishu hiyo alisema: "Mpaka sasa kwenye idara yangu ya habari taarifa hiyo haijafika, nami ninaiona kwenye mitandao, ninasubiri ikifika tutatoa taarifa rasmi juu ya ishu hiyo."

GPL

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
3h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
9h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
12h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’