Mabingwa watetezi michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) Simba leo wanashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Kagera Sugar ukiwa ni mchezo wa hatua ya 16 bora
Ni siku nyingine ya Wanamsimbazi kupata burudani kutoka kwa timu yao
Baada ya kufahamu mpinzani wake kwenye mchezo wa robo fainali michuano ya ligi ya mabingwa, Simba inatumia mechi hizi kama sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo wa kwanza dhidi ya Kaizer Chiefs ambao utapigwa May 14/15 Afrika Kusini
Kocha wa Kagera Sugar Francis Baraza baada ya kipigo cha mabao 2-0 kwenye mchezo wa ligi, alikiri kuwa Simba iko kwenye daraja tofauti sana hivyo anafahamu nini vijana wake wanakwenda kukumbana nacho leo
Habari njema kwa mashabiki wa Simba ni kurejea kwa kiungo Taddeo Lwanga aliyekuwa amesafiri kwao Uganda kwa ajili ya kumzika dada yake aliyefariki wiki iliyopita

Mchezo utapigwa kuanzia saa moja kamili usiku