Afisa Habari wa klabu ya Simba Haji Manara amewataka mashabiki na wadau wamshawishi mlinzi wa kushoto Mohammed Hussein 'Tshabalala' aweze kuongeza mkataba wake aendelee kukipiga na Simba
Jana Tshabalala alifunga bao muhimu la Simba kwa mshuti wenye kasi ya kimbunga jobo katika mchezo dhidi ya Gwambina Fc na akaipeleka Simba kileleni mwa msimamo wa ligi
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Manara amewataka mashabiki kumshawishi nahodha huyo msaidizi aongeze mkataba huku akimsisitizia Boss Lady Barbara Gonzalez aharakishe kumalizana na beki huyo bora zaidi upande wa kushoto hapa Tanzania
Ifikapo mwezi Juni Tshabalala atakuwa amemaliza mkataba wake
Manara ameandika haya;
Kweli msuli huu uende Utopolo ?
Kweli Guu hili la dhahabu likubali kwenda kujitesa kucheza team isiyoshinda mataji ?
Kweli Zimbwe jnr umahiri wa footwork yako na udamwi uliojaalwa ukaupeleke sehemu isiyo na uhakika na kesho yako?
Ww ndio mchezaji unaeimbwa zaidi na Wasanii wa bongo Kwa mahaba yao kwako,,
Ww ni Captain wetu unaependwa ná kila mmoja ndani ya Simba,,
Hii ni timu ya maisha yako,na hapa ndio umekulia na kupata jina lako...
Mm na ww tuliingia pamoja msimu wa 2014 ni mate wangu,,tumetoka mbali na hii klabu,,tunayajua mengi mazuri na changamoto za klabu hii!!
Tumetengeneza bond kubwa na Simba ,,hakuna thamani ya pesa itakayotufanya tuondoke Simba kwenda klabu nyingine ya Tanzania..
Wanasimba wamenituma nikwambie hadharani,,umalizane haraka na uongozi wa klabu kuhusu usajili wako na hawatakubali kukupoteza kwa namna yoyote ile.. sanasana watakuruhusu uende nje ya nchi hii,,sio vtimu vya ajabu ajabu visivyojua kesho yao
Don’t forget,,wanaokushawishi leo walikudhihaki jana,,,usikubali kuiacha team ambayo inakuandaa uwe legendary wake ,na inayokupa furaha kisha ukacheze team usiyoishabikia eti Kwa sababu ya visumni vya kupita ,,furaha na amani ya moyo inazidi rupia za kupita !!
Babra boss wangu,,,,nchi haitatuelewa Zimbwe akiondoka kwenda team za hovyo hovyo ,,Huyu ni Mtoto wa Simba,,limalize hili tuendelee kuonyesha nn Simba inadhamiria ktk muendelezo wa ukubwa wake!!
Naombeni tutangeneze hashtag yoyote ya kumtaka Mohammed Hussein Zimbwe Junior aongeze mkataba @simbasctanzania
@official_mohamedhussein15 @bvrbvra