Mhilu njia nyeupe Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Jun 2020
Mhilu njia nyeupe Yanga

Mshambuliaji Yusufu Mhilu ni miongoni mwa wachezaji wazawa ambao wanatajwa kuwa mbioni kurejea kunako kikosi cha Yanga

Mhilu alilelewa ndani ya Yanga, ni kocha Hans van Pluijm aliyempandisha timu ya wakubwa msimu wa 2016/17

Msimu uliopita Yanga ilimtoa kwa mkopo kwenda klabu ya Ndanda Fc na baadae Mwinyi Zahera kumuondoa kwenye mpango wa kikosi cha msimu huu

Hata hivyo, Mhilu amewathibitishia mabosi wake hao wa zamani kuwa walifanya kumuacha, kwani amekuwa kinara wa mabao katika kikosi cha Kagera Sugar ambacho alitua mwanzoni mwa msimu baada ya kumaliza mkataba wake na Yanga

Ndiye anayeshika nafasi ya pili katika mbio za kuwania ufungaji bora msimu huu, akiwa ameweka kambani mabao 13

Mshambuliaji huyo chipukizi, pia ameifungia Kagera Sugar mabao matatu kwenye michuano ya kombe la FA, pia akiwa na 'asisti' nne

Hapa tunamzungumzia mchezaji ambaye amehusika katika mabao 20 yaliyofungwa na Kagera Sugar msimu huu

Ubora aliionyesha umewavutia mabosi wake wa zamani ambao inaelezwa tayari wamefanya nae mazungumzo na yuko kwenye orodha ya wachezaji watakosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao

cut

Mhilu aliifunga Yanga kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi ambao Kagera Sugar iliibuka na ushindi wa mabao 3-0

Keshokutwa atarejea tena uwanja wa Taifa kuwawinda mabosi wake hao wa zamani kwenye mchezo wa robo fainali kombe la FA

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
13h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
17h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
18h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
18h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’