Nahodha Msaidizi wa Simba Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' amesema Wanasimba waliwaagiza kanda ya ziwa kuchukua alama tisa, sasa wamebakisha alama tatu tu wakamilishe kazi hiyo
Simba imepata ushindi katika michezo miwili waliyocheza kanda ya ziwa dhidi ya Mwadui Fc na Kagera Sugar mchezo ukipigwa jana uwanja wa Kaitaba, Bukoba
Zimbwe Jr mmoja wa wachezaji wa Simba walio katika kiwango bora, amesema siku ya Jumamosi wanakwenda kumaliza kazi waliyotumwa na Wanasimba kule Misungwi ambako watacheza na Gwambina Fc
"Tumepata alama tatu muhimu Kagera, bado alama nyingine tatu Mwanza tuweze kukamilisha kazi tuliyotumwa na Wanasimba huku kanda ya ziwa," alisema Zimbwe Jr
Matokeo ya ushindi dhidi ya Gwambina Fc sio tu yataifanya Simba ishinde michezo yote mitatu kanda ya ziwa, pia yatawapeleka kileleni mwa msimamo wa ligi wakiwaondoa watani zao Yanga