Omog aihofia Mtibwa Sugar, lakini aahidi ushindi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
13 Oct 2017
Omog aihofia Mtibwa Sugar, lakini aahidi ushindi
Vinara wa Ligi Kuu Bara, Simba watakuwa na kubarua kigumu Jumapili mbele ya vinara wenza Mtibwa Sugar katika mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Simba na Mtibwa Sugar zote zinapointi 11, zikitofautiana kwa mabao hali inayofanya makocha wa timu hizo kutazama kwa jicho la tofauti mechi hiyo.

Kocha wa Simba, Joseph Omog alisema mechi hiyo itakuwa ngumu kutoka na Mtibwa kuanza vizuri msimu huu tena kikosi chao kikiwa na wachezaji wenye vipaji licha ya kuondokea na wachezaji wao muhimu msimu huu.

Omog alisema mechi hiyo itakuwa ngumu kutoka na timu zote kuwa na pointi sawa licha ya wao kuwa na idadi kubwa ya magoli na timu itakayopata ushindi kwenye mechi hiyo ndio watakuwa vinara wa ligi jambo ambalo litawafanya kutumia nguvu na maarifa ili kushinda.

“Nimewaona Mtibwa wakicheza na Yanga na walicheza vizuri jambo ambalo limenifanya kuwa na maandalizi kwa umakini ili kutumia mapungufu niliyoyaona kwenye hiyo na kuweza kupata matokeo ya ushindi katika mechi ambayo itakuwa na ushindani dakika zote tisini,” alisema Omog.

“Mtibwa ni moja ya timu nzuri inawachezaji wengi wenye vipaji na wameanza vizuri msimu huu, kwahiyo mechi haitakuwa rahisi kabisa ingawa naendelea na maandalizi vizuri na wachezaji wangu ili kuibuka na pointi tatu ambazo tutaendelea kubaki kileleni,” alisema Omog.

Nahodha wa Simba, Method Mwanjali alisema lengo lao msimu huu ni kufanya vizuri katika ligi, lakini haitakuwa kazi rahisi kwani kila timu wanayokutana nayo watakuwa wanakamia ili wachezaji wao kuonyesha kweli wanacheza na Simba kama ilivyokuwa mechi dhidi ya Mbao Fc.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
9h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
15h ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
18h ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
21h ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
21h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
21h ago
READ MORE →
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE →
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE →
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE →