Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalez ameeleza furaha yake baada ya Simba kumaliza hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa ikiwa kileleni na muhimu zaidi wakionyesha kandanda safi katika mchezo wa mwisho dhidi ya Al Ahly uliopigwa jana, uwanja wa Al Salaam Misri
Barbara amesema Simba walionyesha ukomavu wa hali ya juu katika mchezo huo wakidhihirisha kuwa wameiva sawasawa
"Ninajivunia sana kiwango cha uchezaji wetu kwa sababu tulicheza kama mabingwa. Tumemaliza hatua ya makundi tukiwa kileleni na alama 13. Sasa tunasubiri droo ya robo fainali," alisema Barbara
Licha ya Simba kufungwa bao 1-0 na Al Ahly jana, mabingwa hao wa nchi wamepokea sifa kutoka kila kona kutokana na kiwango kizuri walichoonyesha katika mchezo huo
Huwa sio rahisi sana kufanya vizuri dhidi ya Al Ahly inapokuwa katika uwanja wake wa nyumbani
Simba imedhihirisha kuwa msimu huu wako vizuri na hakika wako tayari kuchuana na yeyote