Habari zilizopatikana viunga vya Jangwani yalipo Makao Makuu ya klabu ya Yanga ni kuwa Katibu Mkuu wa timu hiyo Dk David Luhago amefutwa kazi na uongozi baada ya kushindwa kutimiza majukumu yake
Kwa siku za karibuni Yanga imeonekana kuyumba kiuongozi, baadhi ya wachezaji wakigoma huku kukiwa hakuonekani kuwepo utaratibu wa kuwadhibiti wachezaji wanaozungumza mambo ya ndani ya klabu kwa waandishi wa habari
Aidha tukio la kushindwa kutuma mtu kwenda kumpokea kocha Luc Eyamel aliporejea kutoka Ubelgiji hivi karibuni pia linatajwa kuwa sababu nyingine
Wengi walishangazwa na klabu kubwa kama Yanga kushindwa kutuma mtu wa kwenda kumpokea kocha jambo lililofanya kocha huyo apokelewe na waandishi wa habari ambao pia walimtafutia usafiri wa kumpeleka nyumbani kwake
Bado uongozi wa Yanga haujatoa taarifa rasmi kuhusu hatua hiyo ambayo inadaiwa kuchukuliwa mapema leo