Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) imetangaza kuwa mechi za ligi kuu ya Vodacom zitarejea kuanzia April 08 2021 baada ya kumalizika siku 21 za maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tano, Hayati Dk John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17 2921
Mtendaji wa Bodi hiyo Almas Kasongo amesema kulingana na ratiba iliyotolewa awali, mechi zilizopaswa kupigwa April 06 na 07 sasa zitapigwa April 09 na 10
Hakutakuwa na Mabadiliko ya Ratiba kwa michezo iliyokuwa imepangwa kupigwa April 08
Aidha kutokana na Mabadiliko hayo, michezo ya kombe la FA iliyokuwa ipigwe April 03/04, imefutwa
Kasongo amesema kutokana na changamoto ya muingiliano wa ratiba na mashindano mengine ya Kimataifa, ligi sasa itafikia tamati Julai 11 badala ya Juni 11 iliyokuwa imepangwa awali