Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael anatarajiwa kuwasili nchini leo kuendelea na majukumu yake
Eymael amechelewa kurudi kutokana na changamoto ya usafiri wa ndege huko Ubelgiji iliyosababishwa na ugonjwa wa Covid-19
Aliondoka nchini March 17 baada ya mchezo wa ligi dhidi ya Namungo Fc, ambapo alirejea Ubelgiji kwa ajili ya kufunga ndoa
Licha ya utokuwepo nchini, Eymael aliandaa program za mazoezi ambayo wachezaji walitumiwa wakati wa mapumziko ya corona huku akiwasiliana na kocha msaidizi Charles Mkwasa ambaye tangu wiki iliyopita ndiye msimamizi wa mazoezi ya Yanga
Mbelgiji huyo atakuwa na nafasi ya kukiandaa kikosi chake kabla ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mwadui Fc ambao utapigwa Juni 13 kwenye uwanja wa CCM Kambarage huko Shinyanga
ADVERTISE HERE