Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) limetupilia mbali malalamiko ya klabu ya Al Merrikh iliyodai wachezaji wake nane walibambikiziwa vipimo vya corona visivyo sahihi katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Simba ambao ulipigwa uwanja wa Benjamin Mkapa na Simba kuondoka na ushindi wa mabao 3-0
Wiki iliyopita CAF iliwataka Al Merrikh kuwasilisha ushahidi zaidi wa malalamiko yao jambo ambalo walishindwa kulifanya
CAF imetupilia mbali malalamiko hayo taarifa yao ikieleza kuwa hayana mashiko kwani uchunguzi wao umebainisha kwamba hakukuwepo na udanganyifu wowote wa vipimo
Ndicho kilichotarajiwa kwani vipimo vya corona vinafanyika chini ya uangalizi wa CAF wenyewe, Simba hawakuhusika katika zoezi hilo
ADVERTISE HERE