Baada ya kufanya mazoezi kwa wiki nzima, kikosi cha Yanga kimeanza kuimarika na kuonyesha utayari wa kurejea kwenye mikiki mikiki ya ligi kuu na kombe la FA
Jana mabingwa hao wa kihistoria, walicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Transit Camp inayoshiriki ligi daraja la kwanza
Katika mchezo huo, nyota wa Yanga walionekana kuwa 'fit' na ushindi wa mabao 3-1, ulidhihirisha ubora wao uwanjani
Kumekuwa na ushindani mkali miongoni mwa wachezaji ambapo katika mazoezi, kocha Charles Mkwasa hupanga vikosi viwili na kuvishindanisha
Mkwasa anaamini kikosi chake kiko tayari kurejea kwenye ligi na atautumia mchezo dhidi ya KMC ambao utapigwa keshokutwa, kufanya maboresho ya mwisho kabla ya safari ya mkoani Shinyanga kuifuata Mwadui Fc
ADVERTISE HERE