Gomes awaandalia 'suprise' AS Vita

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
29 Mar 2021
Gomes awaandalia 'suprise' AS Vita

Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema AS Vita wako katika kiwango bora ila anajua ni silaha gani atakayoingia nayo kuwamaliza mapema katika mchezo ujao wa ligi ya mabingwa utakaochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam April 03

Simba wamejipanga kumaliza kazi nyumbani ili mchezo wa mwisho dhidi ya Al Ahly wakacheze wakiwa wamefuzu.

Gomes amesema mchezo huo unaweza kuwa mgumu kutokana na mazingira yake kila timu ikihitaji matokeo ili iweze kusonga mbele hatua ya robo fainali

Aidha amesema AS Vita wamebadilika kulinganisha na walivyokutana nao katika mchezo wa kwanza lakini wanahitaji kwenda na kasi yao ile ile ili kuvuka hatua hiyo

"Ninachoangalia ni hatua ya robo fainali, kama ilivyokuwa kwa michezo iliyopita na hii ni muhimu kwetu kutowadharau wapinzani kwa sababu hivi karibuni wameonesha kiwango kizuri,"; alisema.

Gomes alisema unaweza kuwa mchezo mgumu wenye ushindani ila wao wanahitaji kupata pointi moja tu na lazima wapambane kufa na kupona kuhakikisha wanapata kile wanachokitaka.

Alisema anaamini wachezaji wake watakuwa kwenye kiwango bora na silaha kubwa ni kujiamini na kufanya kile kilichokusudiwa kwa ajili ya kupata matokeo mazuri.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1m ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
11h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’