Leo ni siku nyingine ya huzuni kwa Watanzania ambao wameshuhudia kuzikwa kwa aliyekuwa Rais wao wa awamu ya tano, hayati Dk John Magufuli aliyepumzishwa katika nyumba yake ya milele kwenye makaburi ya familia, Chato
Uongozi wa Simba umeahidi kumuenzi hayati Magufuli kwa vitendo wakiahidi kutimiza agizo aliloacha kwa klabu hiyo mwaka juzi
Katika hafla ya kukabidhi ubingwa wa VPL msimu wa 2018/19, hayati Dk Magufuli aliitaka klabu ya Simba kujiimarisha na kuhakikisha inaleta ubingwa wa Afrika Tanzania

"Lala salama Hayati Dkt. John Pombe Magufuli. Agizo ulilotuachia Simba SC kuwa klabu ya kwanza nchini kuleta ubingwa wa Afrika tutalitekeleza kwa kishindo," ujumbe wa klabu ya Simba baada ya maziko ya hayati Magufuli
April 03 Simba itacheza na AS Vita katika mchezo wa ligi ya mabingwa ambao matokeo ya ushindi au sare yataipeleka Simba robo fainali ya michuano hiyo