Eymael kurejea na mkakati wa ubingwa FA

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Jun 2020
Eymael kurejea na mkakati wa ubingwa FA

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael ni kocha anayeipenda kazi yake na hataki masihara linapokuja suala la majukumu ya kazi

Eymael anasifika kwa kutodumu kwa muda mrefu kwenye vilabu na hii ni kutokana na misimamo yake mikali

Ni juzi tu aliwalaumu viongozi wa Yanga kwa kuchelewa kumtumia tiketi ya ndege ili aweze kurejea nchini

Hata hivyo jana akathibitisha tayari ametumiwa tiketi na kuahidi kuwa mpaka mwishoni mwa wiki atakuwa amewasili nchini

Pamoja na misimamo yake mikali, Eymael ana sifa moja, ni kocha mwenye mafanikio makubwa katika timu alizofundisha

Kocha huyo amekusanya mataji sita ndani ya miaka 10. Ni sifa hiyo iliyomfanya apate ajira ndani ya klabu ya Yanga ambapo gharama zake zote zinalipwa na GSM

Katika malengo yake ya msimu huu, ni kuhakikisha Yanga inashinda taji la FA ili kupata nafasi ya kushiriki michuano ya CAF Confederation msimu ujao

Mbelgiji huyo amesema anahitaji kujenga kikosi imara kwa ajili ya msimu ujao, kupata tiketi ya kushiriki michuano ya CAF kutamrahisishia kuwapata wachezaji anaowataka kwenye timu yake

Pengine hii ndio sababu iliyomfanya awe mkali pale alipoona uongozi wa Yanga unachelewa kumtumia tiketi ili arudi kuwahi kukiandaa kikosi chake

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’