Zaidi ya nusu ya wachezaji wa kikosi cha Simba, wiki hii watakuwa viwanjani wakitimiza majukumu ya Mataifa yao katika michezo ya kuwania tiketi ya kufuzu fainali za Afcon 2021
Simba imeweka rekodi kwa kutoa idadi kubwa ya wachezaji katika timu za Taifa
Wachezaji 18 wamejumuishwa kwenye timu za Taifa kwa ajili ya mechi hizo zinazopigwa mwishoni mwa mwezi huu
Viungo Clatous Chama na Larry Bwalya wako Zambia tayari kuiwakilisha nchi yao wakati Joash Onyango na Francis Kahata wakiwa kule Kenya
Taddeo Lwanga yeye yuko Uganda wakati Peter Muduhwa akiwa kule Malawi
Luis Miquissone yuko kule Msumbiji wakati Meddie Kagere 'MK14' akiwa Rwanda na kikosi cha Amavubi
Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein, Erasto Nyoni, Kennedy Juma, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, Said Ndemla, Hassan Dilunga na John Bocco wao wako na timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' ambayo itashuka dimbani kesho Alhamisi, Guinea ya Ikweta