Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael ameutaka uongozi wa timu hiyo kuharakisha mpango wake wa safari ili arejee nchini kuendelea na majukumu yake
Eymael amethibitisha kuwa tayari safari za ndege nchini Ubelgiji zimeruhusiwa na anachosubiri ni kutumiwa tiketi ya ndege aweze kurejea nchini
Mapema leo Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli alisema kuwa tayari taratibu zote kuhusu safari yake zimekamilika na Mbelgiji huyo ataweza kuwasili nchini wiki hii
"Nimewaomba viongozi wa Yanga wawahi kunitumia tiketi ya ndege niweze kurejea kwani huku safari za ndege tayari zimeruhusiwa. Nimehoji kwa nini mpaka sasa sijatumiwa tiketi wakati ligi imekaribia kuanza. Sijawa na timu kwa zaidi ya miezi miwili hivyo napaswa kurudi mapema ili nipate muda wa kuiandaa timu kabla ya ligi kuanza," alisema Eymael
Inaelezwa baada ya Serikali ya Ubelgiji kufungua safari za anga, ndege nyingi zinazotoka nchini humo zimejaa jambo ambalo limewapa wakati mgumu mabosi wa klabu ya Yanga kupata tiketi
Hata hivyo kwa taarifa iliyotolewa na msemaji wa Yanga mapema leo, ni wazi mchakato wa kupata tiketi ili aweze kurejea umefanikiwa
Β