Kocha Mkuu wa FAR Rabat Sven Vandenbroeck ameeleza kupokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, awamu ya tano, hati Dk John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17 kutokana na matatizo ya moyo
Vandenbroeck aliyekuwa kocha wa klabu ya Simba kabla ya kutimkia Morocco, amesema kifo Dk Magufuli ni pigo kwa Tanzania, Afrika na dunia kwa ujumla
Svena amesema, wakati akiwa hapa Tanzania alishuhudia namna maendeleo ya soka yalivyokuwa yakipambaniwa na watendaji kazi wa Magufuli
"Nawapa pole Watanzania, ni majonzi makubwa kuondokewa na Rais mpendwa wao. pole Tanzania, pumzika kwa amani Magufuli," alisema Sven
Sven alifanya kazi nchin Tanzania kwa takribani mwaka mmoja akiinoa klabu ya Simba kabla ya kutimkia nchini Morocco mwanzoni wa mwaka huu kujiunga na FAR Rabat, moja ya timu zenye historia kubwa nchini humo