Nyota Yanga kutumia fursa ya Laliga, Sevilla

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Jun 2020
Nyota Yanga kutumia fursa ya Laliga, Sevilla

Nahodha wa Yanga Papy Tshishimbi amesema makubaliano ya ushirikiano ambayo Yanga imeingia na wasimamizi wa Ligi Kuu ya Hispania (La Liga) na klabu ya Sevilla, ni fursa kwao

Jana klabu ya Yanga iliandika historia mpya kwa kuingia makubaliano ya ushirikiano na La Liga ambayo yataishuhudia kampuni hiyo inayosimamia vilabu 42 vya ligi kuu na ligi daraja la kwanza nchini Hispania, kushirikiana na Yanga kwenye mchakato wa Mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa mabingwa hao wa kihistoria

Aidha makubaliano hayo pia yameihusisha klabu ya Sevilla ambayo itakuwa na ushirikiano wa moja kwa moja na Yanga, kuanzia timu za vijana mpaka benchi la ufundi

"La Liga ni kampuni kubwa, wanasimamia ligi maarufu duniani. Sevilla ni klabu kubwa imewahi kushinda ligi ya Europa mara tatu mfululizo. Kwetu wachezaji, ushirikiano huu ni fursa nzuri sana kwani inaweza kuwa njia ambayo itatusaidia kupata nafasi ya kwenda kucheza Hispania," alisema Tshishimbi

Aidha Tshishimbi ameongeza kuwa Mabadiliko ya uendeshaji Yanga yataifanya timu hiyo iimarike zaidi kiuchumi, hilo litaongeza ushindani miongoni mwao wachezaji kwani timu itakuwa na uwezo wa kusajili wachezaji bora na wale ambao hawatakuwa na viwango vizuri wanaweza kupoteza nafasi zao

Tshishimbi akiwa nahodha wa Yanga, sambamba na nahodha msaidizi Juma Abdul, walihudhuria hafla hiyo ya kusainiwa mkataba ambayo ilifanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
4h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
20h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’