Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limetaja majina ya waamuzi ambao watachezesha mecho wa ligi ya mabingwa kati ya Simba dhidi ya As Vita utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, April 03
Mwamuzi wa kati ni Haythem Guirat kutoka Tunisia ambaye atasaidiwa na Khalil Hasseni, Yamen Malloulchi na Yousri Bouali wote kutoka Tunisia
Huu ni mchezo ambao Simba inaweza kujihakikishia nafasi ya kutinga robo fainali kama itaondoka na ushindi au hata kupata matokeo ya sare
Baada ya mchezo huu, April 10 Simba itasafiri nchini Misri kuwafuata Al Ahly kwa ajili ya mchezo wa kukamilisha mechi za hatua ya makundi
Simba inaongoza kundi A ikiwa na alama 10, ikifuatiwa na Al Ahly yenye alama saba, AS Vita wako nafasi ya tatu wakiwa na alama nne wakati Al Merrikh wanaburuza mkia wakiwa na alama moja
Alama 11 zitaihakikishia Simba kuvuka robo fainali, hivyo hesabu ni ushindi au sare katika michezo dhidi ya As Vita na Al Ahly
Hata hivyo mchezo dhidi ya Al Ahly ni wazi utakuwa mgumu sana kama Simba itapoteza mchezo dhidi ya As Vita
Vita wakishinda watafikisha alama saba na wanaweza kuvuka robo fainali kama watashinda mchezo wao wa mwisho dhidi ya Al Merrikh ambao utapigwa DR Congo April 10 endapo Simba itafungwa Misri
Kwa hakika mechi ya April 03 AS Vita hapaswi kutoka salama kwa Mkapa, lazima utamaduni wa Mnyama pale kwa Mkapa udumishwe