Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) limewaruhusu wachezaji Ramadan Agabu na Bakhit Khamis kuichezea klabu ya Al Merrikh katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Simba ambao utapigwa kesho Jumanne katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Kwa mujibu wa taarifa iliyopatikana mapema leo, CAF wamesema nyota hao hawakatazwi kuitumikia Al Merrikh kwenye michezo ya ligi ya mabingwa kwa kuwa kifungo chao ni cha ligi ya ndani tu
Wiki iliyopita Simba ilikata rufaa dhidi ya wachezaji hao baada ya kubainika wamefungiwa na Shirikisho la Soka la Sudan kwa kipindi cha miezi sita baada ya kujisajili timu mbili Al Merrikh na Al Hilal
Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema bado hawajapata taarifa rasmi ya CAF, mawazo yao wameyaelekeza katika mchezo wa kesho kuhakikisha wanashinda