Mabingwa wa nchi Simba wamefanikiwa kuondoka na alama moja nchini Sudan baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya Al Merrikh katika mchezo wa ligi ya mabingwa, raundi ya tatu
Simba ilicheza mchezo huo kwa tahadhari lengo likiwa kuondoka na ushindi au sare ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga robo fainali
Huu ni mchezo wa tatu Simba inaondoka na 'cleansheet' katika hatua ya makundi, ikiwa ni rekodi ya kipekee anayoweka kocha Didier Gomes
Sasa El Merrikh wajiandae kuchezea kichapo pale kwa Mkapa, March 16 katika mchezo wa raundi ya nne
Simba imeendelea kubaki kileleni mwa kundi A wakijikusanyia alama saba
ADVERTISE HERE