Onyango 'kuwakera' wanaomuita Mzee

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
2 Mar 2021
Onyango 'kuwakera' wanaomuita Mzee

Beki kisiki wa Simba, Mkenya Joash Onyango, amesema anakaribia kuweka tena rangi nyeupe kwenye ndevu zake ili zionekane ana mvi mithili ya mzee kama alivyowahi kufanya akiwa nchini Kenya

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Onyango alisema baada ya mechi tatu au nne, ataweka tena rangi nyeupe ndevu zake kwa ajili ya kuwatumia salamu wajukuu zake.

Onyango alifafanua kuwa wajukuu zake ni wale waliokuwa wakimbeza kuwa yeye ni mzee na klabu ya Simba imesajili mchezaji mwenye umri mkubwa.

"Nakaribia kuzirudisha tena ndevu zangu nyeupe, sasa niwe babu kabisa kwa wajukuu zangu, niwatumie salamu," alisema Onyango.

Kabla ya kujiunga na Simba, Onyango alikuwa gumzo akiwa kwenye kikosi cha Harambee Stars ya Kenya, alipoamua kupaka rangi nyeupe ndevu zake na kuonekana kama mzee, na hata alipojiunga na Klabu ya Simba, picha zake hizo zilitumika na mashabiki wengi wakibeza usajili wake.

Wakati Onyango akitaka kurudisha mvi zake, tayari mashabiki wa Tanzania wameshabadilisha mtazamo na kumchukulia kuwa ni mmoja wa mabeki bora kabisa nchini kwa sasa.

Kuhusu hali ya usajili wake kubezwa, Onyango alisema kuwa hawezi kumlaumu mtu yoyote kwani kila mtu ana mtazamo wake.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
3h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
9h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
12h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’