Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela ameeleza kutounga mkono kupunguza idadi ya nyota wa kigeni akibainisha sheria hiyo itakwenda kuviathiri vilabu vitatu tu Yanga, Simba na Azam Fc ambazo ndizo zenye uwezo wa kusajili wachezaji 10
Mwakalebela amesema idadi ya nyota wa kigeni nchini hawazidi 60, ukiondoa Yanga, Simba na Azam Fc, baadhi ya timu hazina wachezaji wa kigeni huku chache zikiwa na wachezaji chini ya watano
"Timu tatu tu ndizo zenye uwezo wa kusajili wachezaji 10 ambazo ni Simba, Yanga na Azam na husaidia kuleta ushindani kwa wazawa sasa tukiwapunguza tutawadumaza hawa wa ndani na sasa soka siyo ridhaa japo sheria inatambua hivyo nayo imepitwa na wakati," amesema
Mwakalebela alatoa ushauri kwa serikali kutotunga Sera kwa kuangalia klabu tatu pekee kwani kutawaumiza wanaokwenda kushindana kimataifa
Pia amehoji hatma ya wachezaji wenye mikataba ya muda mrefu watakwenda wapi kama timu zitatakiwa kupunguza idadi