Manara amtuza Ajibu kwa 'kukichafua' mechi ya African Lyon

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
27 Feb 2021
Manara amtuza Ajibu kwa 'kukichafua' mechi ya African Lyon

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Haji Manara, amemzawadia kiungo mshambuliaji Ibrahim Ajibu fedha taslim Tsh Milioni Moja baada ya kuonyesha kiwango bora kwenye mchezo wa raundi ya nne kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya African Lyon

Mchezo huo uliopigwa jana katika uwanja wa Benjamin Mkapa, uliwashuhudia mabingwa wa nchi Simba wakiondoka na ushindi wa mabao 3-0 na hivyo kutinga hatua inayofuata kibabe

Ajibu ndiye aliyekuwa nyota wa mchezo huo akiweka kambani mabao mawili huku akionyesha kiwango bora

Manara alieleza kuvutiwa na uwezo alioonyesha Ajibu na kuamua kumtuza kiasi hicho cha fedha

"Hivi ndivyo Wanasimba wanataka. Ibrahim Ajibu soma muamala wako kuna kamilioni nimekasendi kwenye Simu yako. Nimekutumia na ya kutolea," aliandika Manara kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii

Baadae Ajibu alithibitisha kupokea kiasi hicho cha fedha; "Bugatti Nimeshapokea muamala. Shukrani sana kaka"

Ajibu amekosa nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha Simba, hata hivyo amefanya vizuri kila alipopewa nafasi

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
15m ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
3h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
8h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
23h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’