Beki wa zamani wa Yanga Hassani Kessy ambaye sasa anaichezea klabu ya Nkana Fc ya Zambia, yuko ukiongoni mwa mkataba wake unaomalizika mwishoni mwa msimu
Kessy amesema Nkana bado hawajampa ofa mpya hivyo amefungua milango kwa timu ambazo zingependa kufanya nae kazi
"Mkataba wangu unamalizika mwishoni mwa msimu, bado sijaanza mazungumzo na Nkana lakini niko huru kupokea ofa kutoka timu nyingine," amesema
Upo uwekezekano mkubwa Kessy hataongeza mkataba Nkana baada ya timu hiyo kudaiwa kukumbwa na ukata unaopelekea wachezaji wengi kuamua 'kusepa'
Katika nafasi ambazo Yanga huenda ikaongeza nguvu ni pamoja na walinzi wa pembeni
Kama vipi si arejeshwe Jangwani huyu mwamba?
ADVERTISE HERE