Miquissone awapagawisha waarabu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
25 Feb 2021
Miquissone awapagawisha waarabu

Inaelezwa klabu ya Al Ahly inajipanga kuwasilisha ofa nono kwa klabu ya Simba wakitaka kumsajili winga Luis Miquissone

Miquissone alikuwa mwiba mkali dhidi ya wababe hao wa soka barani Afrika juzi, akifunga bao pekee lililoihakikishia Simba kuondoka na alama zote tatu baada ya ushindi wa bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Kama mpango huo utakamilika Simba inatarajiwa kuvuna kitita kikubwa cha fedha

Msemaji wa Simba Haji Manara amesema klabu haitakuwa na kinyomgo kumuacha nyota huyo aondoke kama watapokea ofa nono

"Mpira ni kazi yake, sisi hatuwezi kumzuia kama itatokea timu ikampa maslahi zaidi kuliko sisi. Lakini hata hivyo kwa sasa Miquissone ni mchezaji ghali sana hivyo kwa yeyote anayetaka kumsajili inabidi ajipange sawasawa," alisema Manara

Aidha bosi huyo wa kitengo cha habari klabu ya Simba, amesema sio Al Ahly tu, wamepokea ofa kutoka timu nyingine ndani ya Afrika na hata nje ya bara la Afrika

Tangu ajiunge na Simba mwishoni mwa mwaka uliopita, Miquissone amekuwa katika kiwango bora

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
43m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
22h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’