Keshokutwa Jumanne Simba inakabiliwa na mchezo muhimu wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Ahly
Ni mchezo ambao matokeo ya ushindi kwa Simba, sio tu yatawapeleka kileleni mwa kundi A, lakini pia yatawaweka katika nafasi nzuri ya kutinga robo fainali kwani mabingwa hao wa nchi watahitaji angalau alama nyingine tatu au nne kuweza kutinga robo fainali
Kuelekea mchezo huo, Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amesema amekuwa akiwafuatilia Al ahly kwa wiki kadhaa akipitia michezo yao waliyocheza
Gomes amefichua kuwa amebaini uimara wao na pia amegundua madhaifu yao, na sasa anawaandaa wachezaji wake kuweza kukabiliana nao Jumanne
"Nimeangalia mechi zao nyingi kubaini vile wanavyocheza katika kushambuliaji na safu yao ya ulinzi. Tumeona ubora wao uko wapi na pia madhaifu yao. Tutatumia hiyo kama silaha kuweza kuwafunga," alisema Gomes
"Tunaendelea kuwaandaa wachezaji wetu kimbinu kuhakikisha kila mmoja anafahamu nini anapaswa kufanya katika mchezo huo ili tuweze kufanikisha lengo letu"
"Nimefanya vikao na wenzangu wa benchi la ufundi pamoja na wachezaji ili kuona mpango wetu tunaweza kuufanikisha kikamilifu"
Al Ahly ndio mabingwa watetezi, pia wakiwa mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo ya ligi ya mabingwa
Hivi karibuni wametokea kule Qatar kushiriki michuano ya kombe la dunia la vilabu wakifanikiwa kuibuka katika nafasi ya tatu
Katika michuano hiyo walifungwa na Bayern Munich, mabingwa wa Ulaya mabao 2-0
Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema wanatambua ugumu wa mchezo dhidi ya Al Ahly lakini kama ilivyo kaulimbiu ya kuelekea mchezo huo, ni vita kamili ambayo wanapaswa kushinda
Lakini pia ni historia, Simba haijawahi kufungwa na Al Ahly hapa Tanzania, wameshinda mechi zote mbili walizocheza nchini
Mchezo wa Jumanne utakuwa wa tatu kwa Simba kuondoka na alama zote tatu dhidi ya Al Ahly, hili ndilo lengo la Simba