Mabingwa wa nchi Simba wanaendelea kusogea katika nafasi yao baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Biashara United katika mchezo uliopigwa uwanja wa Karume, Musoma
Bernard Morrison 'Mzee wa kuwakeraaaa' ndiye aliyeihakikishia Simba ushindi muhimu kwa bao safi la dakika ya 22 akifunga bao hilo baada ya kuvunja mtego wa kuotea
Ulikuwa mchezo ambao Morrison angefunga mabao matatu kama angeweza kutumia nafasi nyingine mbili za wazi alizopata
Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes alifanya mabadiliko ya kikosi chake akiwapa mapumziko baadhi ya nyota muhimu
Ulikuwa mkakati wa kuhakikisha anakuwa na kikosi chake kamili katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Ahly utakaopigwa Februari 23
Mabingwa hao wa nchi wameendelea kusogea karibu kabisa na nafasi ya kwanza sasa wakifikisha alama 42 baada ya kushuka dimbani mara 18
Ni alama nne tu zimesalia kufika pale juu huku Simba wakiwa na mechi mbili mkononi
Sasa nguvu zinahamishiwa kwenye mchezo dhidi ya Al Ahly, mwarabu lazima akae pale kwa Mkapa Februari 23