Nugaz ataka VAR iharakishwe Tanzania

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 May 2020
Nugaz ataka VAR iharakishwe Tanzania

Afisa Mhamasishaji wa klabu ya Yanga Antonio Nugaz amesema anaamini nchi za Afrika ikiwemo Tanzania haziwezi kukwepa matumizi ya teknolojia ya VAR katika ligi zao

VAR ilianza kutumika kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka 2018 na sasa ligi karibu zote barani Ulaya zinatumia teknolojia hiyo kuwasaidia waamuzi

Barani Afrika nchi ya Morocco tayari imeanza kutumia kwenye ligi yao huku Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) likitumia teknolojia hiyo kwenye michuano ya ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho kuanzia hatua ya nusu fainali

Nugaz amesema kama VAR italetwa Tanzania basi itaondoa yale 'makandokando' mengi yanayoonekana katika ligi yetu

"Kama imeanza kutumika barani ulaya, nadhani na sisi Afrika ni wakati  wetu kuangalia matumizi ya teknolojia hiyo. VAR itasaidia kutenda haki na kuondoa uonevu kutokana maamuzi yasiyo sahihi. Hapa kwetu itaondoa yale makandokando mengi ambayo yanaonekana kwenye ligi yetu," amesema

Msimu huu malalamiko mengi yameelekezwa kwa waamuzi ambao wengi wameonekana kushindwa kuzitafsiri kwa usahihi sheria 17 za mchezo wa soka

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’