Raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika imekamilika usiku wa kuamkia leo kwa mchezo mmoja wa kundi A kati ya Al Ahly dhidi ya Al Mareikh ya nchini Sudan
Mchezo huo umechelewa kupigwa kutokana na Al Ahly kukabiliwa na michuano ya klabu bingwa ya dunia iliyofanyika nchini Qatar, mabingwa hao wa Afrika wakimaliza katika nafasi ya tatu
Jana wamewafumua Al Mareikh mabao 3-0 na kuungana na Simba kuwa timu pekee zilizoshinda mechi zao za kwanza kundi A
Ushindi huo umewaweka Al Ahly kileleni mwa kundi A kwa tofauti ya mabao, Al Ahly wakiwa na mabao matatu huku Simba ikisalia nafasi ya pili kutokana na ushindi wake wa bao 1-0 dhidi ya AS Vita
Michezo ya raundi ya pili itapigwa wiki ijayo, Februari 23 Simba ikishuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Al Ahly wakati AS Vita watasafiri nchini Sudan kuwakabili Al Mareikh
Hii ni vita kati ya vinara wa kundi na vibonde wa kundi...!