Mabingwa wa nchi Simba wameanza vyema hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kuichapa AS Vita bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Stade de Martyrs nchini Congo
Chris Muchimba Mugalu ndiye aliyeihakikishia Simba ushindi muhimu ugenini kwa bao la mkwaju wa penati katika dakika ya 60
Chama alimwekea Luis Miquissone pasi murua ndani ya eneo la hatari akaachia mkwaju ambao ulimgonga mkononi mlinzi wa AS Vita na hivyo mwamuzi kuamuru mkwaju wa penati



Ulikuwa ni mchezo ambao mbinu za kocha Didier Gomes zilifanikiwa zaidi kwani kwa mara ya kwanza tumeishuhudia Simba ambayo iko makini sana kwenye ulinzi
Kila mchezaji alitimiza majukumu yake hasa pale walipopoteza mpira, hakukuna na nafasi zilizoachwa wazi hali iliyowapelekea AS Vita wakati mgumu mbele ya lango la Simba
Ni ushindi ambao umeiweka Simba katika nafasi nzuri ya kurudia kile walichokifanya mwaka juzi, kwani ushindi katika mechi nyingine mbili, kimahesabu unaweza kuipeleka Simba robo fainali
Mchezo unaofuata ni dhidi ya Al Ahly na utapigwa Februari 23 uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam
Habari ziwafikie wale waliokuwa wakiamini Simba haiwezi kushinda ugenini
Mwaka huu Wanamsimbazi wana jambo lao katika michuano ya ligi ya mabingwa....!