Yanga inahitaji muda kuwa sawa - Niyonzima

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Apr 2020
Yanga inahitaji muda kuwa sawa - Niyonzima

Kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima amesema kikosi cha timu hiyo kina wachezaji wengi wazuri lakini watahitaji muda ili kuzoeana

Nahodha huyo wa timu ya Taifa ya Rwanda, amesema wanahitaji kucheza pamoja kwa muda ili watengeneza muunganiko mzuri

Niyonzima amekumbushia kikosi kilichotwaa taji la ligi kuu kwa misimu mitatu mfululizo kuanzia mwaka 2014 mpaka 2017 kuwa walicheza pamoja kwa muda mrefu na hivyo kuzoeana

"Yanga tulichukua kikombe cha Ligi Kuu Bara mara tatu mfululizo, sio kama tulikuwa na kikosi hatari sana, lakini tulizoeana, mchezaji unajua ukipeleka mpira hapa, utamkuta mwenzako, huwezi kupata mafanikio haraka haraka," amesema

Niyonzima aliyerejea Yanga usajili wa dirisha dogo akitokea AS Kigali ya kwao Rwanda, amesema uamuzi wa kurejea kwa mabingwa hao wa kihistoria haukuangalia maslahi zaidi bali ni kwa sababu ndio timu anayoiheshimu zaidi nchini

"Nimerudi Yanga kwa sababu ndio timu ninayoiheshimu na ni timu ninayoifurahia, ni kweli tunaangalia maslahi, lakini lazima uwe na sababu zako binafsi, kwa hisia zangu binafsi ndio zilipelekea kukubali kurejea"

Niyonzima amesema alipata nafasi ya kucheza Simba kwa misimu miwili lakini hakupata mafanikio kutokana na changamoto ya majeruhi ya mara kwa mara. Hata hivyo amesema hafikirii tena kama iko siku atarejea kuitumikia timu hiyo

"Siku zote tunaishi kwa kumtegemea Mungu. Nilimuomba mungu niweze kurudi Yanga, na namuomba mungu anisaidie ili nizidi kufanya vizuri hapa. Sidhani kama itatokea siku nitarudi kuichezea Simba"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
9h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’