Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Haji Manara amewataka mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kuendelea kuiunga mkono timu yao katika michezo ijayo na kuwa wasikatishwe tamaa na matokeo ya sare dhidi ya Azam Fc
Manara amesema waliingia katika mchezo huo wakiwa na malengo ya kushinda lakini haikuwa hivyo, wanapaswa kusonga mbele kuelekeza nguvu zao katika mechi zijazo
"Jana kila mmoja alitarajia tungeshinda. Kipindi cha kwanza tulicheza vizuri sana, tulitengeneza nafasi nyingi lakini tukatumia nafasi moja. Kipindi cha pili wenzetu walijipanga nao wakarejea wakiwa imara. Ndivyo mpira ulivyo, kuna wakati tutashinda, tutadroo na nyakati nyingine tutafungwa"
"Hatuna sababu ya kulaumiana kwani ni matokeo ya mpira ambayo kila timu lazima iyapate. Sisi lengo letu ni kutetea ubingwa, bado naamini tutalifanikisha hilo muhimu tunapaswa kuendelea kuwa wamoja na kuiunga mkono timu yetu," alisema Manara
Mchezo huo uliomalizika kwa matokeo ya sare ya mabao 2-2, uliishuhudia Simba ikitawala kipindi cha kwanza lakini ikishindwa kutumia nafasi kufunga mabao. Meddie Kagere alifunga bao pekee katika kipindi hicho huku Clatous Chama akikosa mkwaju wa penati
Kipindi cha pili Azam Fc walizinduka na wakafanikiwa kufunga mabao mawili kupitia kwa Iddi Selemani Nado na Ayubu Lyanga kabla Luis Miquissone hajaisawazishia Simba kwa bao la shuti kali kutoka nje ya 18