Keshokutwa Jumatano Simba itashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Al Hilal kutoka nchini Sudan katika mchezo maalum wa michuano ya Simba Super Cup utakaopigwa kuanzia saa 11 jioni
Tayari tiketi za kushuhudia mchezo huo zimeanza kuuzwa katika vituo vilivyoainishwa na klabu ya Simba

Simba ilianza kujifua juzi kujiandaa na michuano hiyo, jana wakimpokea kocha mkuu Didier Gomes aliyetokea kule Sudan klabu ya El Marreikh
Mfaransa huyo hakupoteza muda kwani jana jioni alianza kukiandaa kikosi chake tayari kwa michuano hiyo maalumu iliyoandaliwa na Simba ikizihusish Al Hilal na TP Mazembe kutoka DR Congo
ADVERTISE HERE