Mwakalebela awavuruga Simba, watishia kwenda FIFA

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Apr 2020
Mwakalebela awavuruga Simba, watishia kwenda FIFA

Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amesema klabu hiyo itapeleka malalamiko TFF na FIFA kwa kitendo cha klabu ya Yanga kutaka kumsajili kiungo wao Clatous Chama bila ya kufuata utaratibu

Akihojiwa kwenye chombo kimoja cha habari mapema leo, Manara alidai Chama ana mkataba wa zaidi ya miezi sita na klabu ya Simba hivyo timu yoyote inayotaka kumsajili bila kufuata utaratibu inafanya makosa

Jana Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela alifichua kuwa walikuwa wakimfuatilia nyota huyo ambaye alidai kuwathibitishia kuwa mkataba wake uliobaki ni chini ya miezi sita

Manara amesema watachukua hatua

"Tutaiandika barua TFF kuhusu Mwakalebela kuongea na mchezaji wetu mwenye mkataba na kuvunja kanuni za ligi, katika suala hili hatuwezi kukaa kimya," alisema Manara

Alichosema Mwakalebela;

Mwakalebela alisema wanaamini, Chama amebakiza mkataba wa miezi sita (6) tofauti na klabu ya Simba inavyosema kwamba bado mchezaji huyo anamkataba wa miaka miwili.

"Wenzetu wameweka dau wamesema wanataka Dola za Marekani 350,000 ili kumpata Chama ingawa tunajua kabisa amemaliza mkataba. Ningependa kusema kwamba, tunafatilia kwa karibu na tumeanza mazungumzo na Chama na ikiwezekana tungependa aweze kuchezea Yanga"

"Kama tutakubaliana vigezo na masharti ambayo ameyatoa yeye basi atakuwa mchezaji wetu. Nisingependa niwahakikishie wapenzi na wanachama wa Yanga kwamba tayari tumeshasaini mkataba, nitakuwa nawadanganya ila tunamuhitaji na tunamfatilia na tunaendelea kuwa na mazungumzo naye kama tutafikia mwafaka mzuri tutamleta klabuni kwetu"

"Kwa mujibu wa maelezo yake mkataba wake unaisha ndani ya miezi sita (6) ijayo, Simba wanasema anamkataba wa miaka miwili (2) kwa hiyo inamaanisha alisaini miaka minne (4) kitu ambacho sisi hatukiamini kama ni kweli"

"Simba kama wanauhakika watueleze kwamba wanamkataba wa miaka miwili (2) lakini sisi tunaruhusiwa kuongea na mchezaji akiwa amebakiza mkataba wa miezi (6) na ndicho ambacho sisi tunafanya. Kama wanauthibitisho tutapeleka posa kwa barua kama inavyotakiwa"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
9h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’