Tanzania yaichapa Namibia 1-0

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
23 Jan 2021
Tanzania yaichapa Namibia 1-0

Tanzania leo imejitutumua mbele ya Namibia baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa pili kundi D, michuano ya CHAN

Bao la Farid Mussa aliloweka kambani kwenye dakika ya 65 liliihakikishia Tanzania ushindi muhimu ambao unaweka hai matumaini ya kufuzu hatua ya mtoano

Tanzania ilitawala mchezo huo kwenye kipindi cha kwanza, wakitumia mipira mirefu ambayo ilikuwa ikiwapa changamoto walinzi wa Namibia

Katika kipindi cha pili Namibia walirejea wakiwa bora zaidi lakini kazi nzuri iliyofanywa na Ayubu Lyanga, aliyepiga krosi maridhawa ambayo ilitua kichwani kwa Ditram Nchimbi aliyemtengea Farid kufunga bao hilo muhimu

Kazi nzuri pia ilifanywa na mlindao lango wa Tanzania Aishi Manula ambaye aliliweka lango la Stars salama wakati Namibia wakiweka presha kusaka bao la kusawazisha

Tanzania sasa inahitaji kushinda mchezo wa mwisho dhidi ya Guinea ili kuweza kutinga hatua ya robo fainali

Katika mchezo wa mapema, Zambia na Guinea zilitoshana nguvu baada ya kutoka sare ya bao 1-1

Guinea inaongoza kundi ikiwa na alama nne sawa na Zambia timu hizo zikitofautiana bao moja

Tanzania inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama tatu wakati Namibia imeyaaga mashindano hayo baada ya kipigo cha leo

Katika mchezo wa Namibia dhidi ya Tanzania, Farid Mussa aliondoka na tuzo ya nyota wa mchezo huo

 

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
4h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
7h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’