Hakuna haraka kurejesha shughuli za soka - FIFA

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Apr 2020
Hakuna haraka kurejesha shughuli za soka - FIFA

Wakati siku nne zikiwa zimesalia kumalizika kwa siku 30 zilizotolewa na Serikali kusitisha shughuli zote za michezo nchini kutokana na janga la corona, upo uwezekano mkubwa Serikali itaongeza muda wa katazo hilo kutokana na mwenendo wa maambukizi ya virusi vya corona nchini

Tayari Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limebainisha kuwa ratiba zake zote za saka nchini hazitaendelea hadi pale Serikali itakapotoa ruhusa

Aidha Shirikisho la soka duniani (FIFA) kupitia Rais wake Gian Infantino, limeshauri kuwa nchi hazipaswi kuharakisha kurejesha ligi zao kabla ya kujiridhisha na hali ya usalama wa raia wake kutokana na janga la corona

"Hakuna mechi, hakuna mashindano, hakuna ligi ni bora kujali maisha ya wanadamu, ni vizuri tukasubiri zaidi kuliko kujiweka katika hatari," alisema

Soka linaendelea katika mataifa machache kama vile Belarus, Burundi, Nicaragua na Tajikistan. Infantino, aamesisitiza kuwa usalama unatakiwa kutangulia kwanza na mengine yatafuatia.

"Kila mmoja kichwani mwake lazima kuwe na mawazo ya janga hili, itakuwa zaidi ya kutowajibika endapo kutakuwa na kulazimisha kufanyika kwa mashindano kama mambo hayako salama kwa asilimia 100, "alisema Infantino.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’