Timu ya Taifa ya Tanzania, leo itashuka dimbani pale Cameroon kupepetana na Zambia katika mchezo wa kundi D fainali za michuano ya CHAN 2021
Ni mchezo ambao vijana wa kocha Etienne Ndayiragije wanahitaji kuanza vyema ili kuwa na matumaini ya kufanya vizuri katika michuano ya mwaka huu
Meneja wa Stars Nadir Haroub, amesema wachezaji wote wana ari kuelekea mchezo huo
Amesema kila mmoja anafahamu umuhimu wa kuanza vyema michuano hiyo lakini pia ni nafasi kwao wachezaji kujitangaza kwani wanaangaliwa na Mawakala kutoka kila kona ya dunia
Mchezo utapigwa kuanzia saa moja usiku kwa saa za Afrika ya Mashariki
ADVERTISE HERE