Maandalizi ya mapema ni muhimu ligi ya mabingwa - Matola

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
18 Jan 2021
Maandalizi ya mapema ni muhimu ligi ya mabingwa - Matola

Kocha Msaidizi wa Simba Selemani Matola amesema wanahitaji kufanya maandalizi ya mapema kujiandaa na hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Baada ya timu kupangwa kwenye makundi zinarudi Februari kucheza hatua hiyo kutafuta nafasi ya kuingia robo fainali katika michuano hiyo mikubwa barani Afrika

Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Matola alisema anatambua ugumu wa michuano ile ila hana wasiwasi kwasababu wachezaji alionao wengi ni wazoefu na waliwahi kucheza msimu wa mwaka juzi

"Kundi letu ni gumu sio rahisi kwasababu kule huendi kukutana na mtu mdhaifu, ni timu zilizojiandaa ndio maana tunahitaji kuandaa timu mapema kwa ajili ya mashindano hayo," alisema

Simba baada ya kuingia hatua ya makundi Kocha wake Mkuu Sven Vanderbroeck aliachana na timu hiyo baada ya kupata dili la kuifundisha klabu ya AS FAR ya Morocco

Matola alisema katika kuelekea huko wachezaji pia, wanatakiwa wajitambue na kujipanga kwenda kupambana ili kukabiliana na yeyote kwa ajili ya kupata matokeo mazuri.

Simba inatarajiwa kufungua dimba dhidi ya AS Vita katika mchezo wa kwanza utakaochezwa Februari 12, mwaka huu nchini DR Congo

Baadaye watacheza nyumbani dhidi ya Al Ahly Februari 23, mwaka huu kisha Machi kucheza na Al-Merrikh ugenini na kumaliza mzungumko wa kwanza kabla ya baadaye kurudiana wa pili.

Mbali na Simba, timu nyingine inayowakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa ni Namungo inayoshiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18m ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
12h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’